Mon Feb 03 - Written by: Kups
About me and this blog
Maneno machache ya kutuget acquainted na each other.
Niaje!
Mimi ni Kups, na kama wewe, nimekuwa nikitry kusoma more books this year kushinda last year. Lakini kwanini nimeamua kuanza blog 2025? Soma zaidi kujua!
Mimi ni nani?
Siwezi jiconsider an established author but juu nimeslide kwa DM’s kadhaa naweza sema kidogo I know my way around words. Jokes, aside, in not so many words, mimi ni yule jamaa huitwa a jack of all trades, but a master of none. I hope bado tunakubaliwa kutumia the word master, seeing vile siku hizi watu huget offended virahisi. Pole, I digress. Nilikuwa nasema, najua kufanya vitu kadhaa, kama kuandika code. I mean ndo maana nimecreate hii blog. Wale wako nerdy kidogo wanaweza tell sijatumia Wordpress na the likes. Besides code, naweza design kidogo, thanks to experience ya kutengeneza web applications for almost 10 years now. Kuandika something this long, mara ya mwisho ilikuwa insha za high school so mtaniwia radhi kama nitajipata nastruggle kufikisha a thousand words ama nikijirudia sana. Acha nianze a new paragraph. Kando ya hizi vitu nimetaja hapa juu, napenda kusoma any chance I get. From non-fiction, to fiction, Western to Eastern to African literature. I think vitu sijasoma sana ni comics na manga. All in all, hii blog ni a way to combine these 3 skills while living my mantra ya kugrow a little kila siku.
More on mbona a blog in 2025?
Yeah najua vile siku hizi watu huspend most of their time kwa social media kama IG na TikTok as well as X. So kwa nini nisitumie hizo platforms kuconnect na audience. The easy explanation ni that nataka kutenga a corner kwa internet kwenye I can be putting down my thoughts and ideas as well as kushare the things nitakuwa nimelearn from a book I am reading at that moment. Whether kutakuwa na mtu on the other side of the screen akisoma these words, sijui. Labda nikifigure out vile nitaweka comment section, nitajua sio mimi pekee nasoma hizi words.
The other reason ni, hii blog itakuwa one of the ways ya kujikeep accountable so that nisome more books than last year. Last year, nilikuwa na goal ya kusoma 20 books. Mwaka ukaisha kama nimesoma tano. So najipush kthis year kusoma 15, ndio nimalize mwaka kama nimesoma 10. Si hio inamake sense? 😂
One other thing ni, books have been instrumental in shaping attitude yangu towards life. Mnakumbuka sisi wote tulikuwa lockdown a few years back bila ya kuweza kusocialize kama kawaida na out friends. Having been msee nilikuwa nimezoe sherehe na kuchase the next high, hii time ilikuwa a new experience for me bila the tools to handle it. Vile Lilmaina husema, it wasn’t long before ki-depression ikick in. Well for me it was more of anxiety. Rediscovering that I enjoyed reading, kuna vitabu fulani nilisoma zikanisaidia kunavigate hio period vipoa na naweza sema since then sijawahi worry much about what the future holds. One of this day I will summarize some of the books that helped me the most.
Mwishowe I think most people pia hawana time ya kusoma hundreds of pages just to see whether a book is worth reading so I am hopiong with my distilled summaries, nitakusaidia kumake a decision whether unadai kuget hio book or not.
Kumalizia
Hoping over time, my writing itaget better. I mean one of my mantra ni “asilimia moja kila siku”. Growth mentality ka hii itakuwa instrumental kwangu kufanikisha goals niko nazo. Karibu to my corner of the internet. Hopefully tutainteract more over time nikishaweka hio comment section. Kama umefika mwisho wa hii kitu, hebu enda kaache comment kwa hii post pale IG ndo nijue niko na msomi at least mmoja. Unaweza include the word “mtondogoo” kwa comment yako ndo nijue kwenye umetoka pamoja na what your current or next read is?
Lemme leave you with one quote till the next time! Shukran!
A reader lives a thousand lives before he dies… The man who never reads lives only one. — George R.R. Martin